Mahakama kuu ya Kenya imesema haina uwezo kisheria kuamua kama wagombea
urais katika uchaguzi ujao nchini humo, Uhuru Kenyatta na mgombea wake
mwenza William Ruto, waendelee kugombea au la.
Jopo la majaji watano wa mahakama hiyo, wamesema kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kushughulikia suala linalohusu kugombea urais, wakisema ni mahakama ya juu kabisa pekee ambayo inao uwezo huo.
Viongozi hao wa Muungano wa Jubilee wamepata afueni sasa baada ya Mahakama Kuu kuhamishia kesi hiyo kwenye Mahakama ya Juu.
Mahakama hiyo imesema kwa kuwa tayari Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imeshakubali uteuzi wa Kenyatta na Rutto kushiriki kwenye uchaguzi mkuu ujao, mahakama hiyo haina mamlaka ya kubadilisha uamuzi wa IEBC.
Mahakama hiyo imesma kwamba inao tu uwezo wa kuchunguza upya uamuzi wa
IEBC kuhusu wagombea wengine lakini si wagombea urais na wagombea wenza
wao.
ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 nchini KENYA.
Mahakama hiyo imesema kwamba wawili hao hawana hatia hadi
watakapohukumiwa katika kesi yao inayowakabili huko The Hague na hakuna
mtu anayeweza kubashiri iwapo wawili hao watapatikana na hatia.
Kesi hiyo ilifunguliwa na vyama vya kiraia vikipinga ushiriki wa wawili hao katika uchaguzi wa hapo tarehe 4 Machi, kwa madai kuwa wamekosa uadilifu kwa sababu wagombea hao tayari wamefunguliwa mashtaka ya kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).
Mahakama hiyo imesema kwamba endapo mahakama ya ICC ingewasimamisha
wawili hao kugombea nyadhifa za uongozi, basi hilo lingeliwezekana.
Mahakama hiyo imeamua gharama ya washtakiwa kwenye kesi hiyo ilipwe na
wenye kushtaki.
No comments:
Post a Comment