Friday, February 15, 2013

HATMA YA WASHUKIWA WA ICC KUGOMBEA KENYA

         Uamuzi unatarajiwa kutolewa wakati wowote kuanzia sasa kuhusu iwapo wagombe wawili katika uchaguzi mkuu Kenya Uhuru Kenyatta na William Ruto wanapaswa kugombea nyadhifa.
Uhuru kenyata anawania uraisi katika uchaguzi mkuu unaowadia katika muda wa wiki mbili zijazo na naibu 
 wake ni William Rutto
 
 Uamuzi kuafikiwa ikiwa wawili hawa watawania nyadhiza za rais na makamu wake

Kesi hiyo iliyowasilishwa na mashirika yasiyo ya kiserikali inaendelea katika mahakama kuu mjini Nairobi na inatarajiwa kutoa uamuzi iwapo mahakama ina uwezo wa kutoa uamuzi juu ya wawili hao au iwapo itahitaji usaidizi wa mahakama ya juu nchini kufikia uamuzi kuhusu hilo.
Hii ni wakati zimesalia wiki mbili tu kwa uchaguzi mkuu kufanyika Kenya na uamuzi huu huenda ukawa na athari kubwa kwa uchaguzi ujao.
         Mahakama inajaribu kuona iwapo Uhuru na Ruto ikiwa watachaguliwa wataweza kutimiza jukumu la kuiongoza nchi, na wakati huo huo kukabiliana na kesi inayowaandama katika mahakama ya uhalifu wa kivita ICC mjini Hague Uholanzi, ambapo wanatuhumiwa kuhusika na ghasia zilizoshuhudiwa baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.

No comments:

Post a Comment