Kiongozi wa Ujumbe wa waangalizi wa Umoja wa Afrika, Joachim Chissano
ameishauri tume huru ya uchaguzi nchini Kenya IEBC kushirikiana na
vyombo vya usalama kuhakikisha uchaguzi ujao unakuwa wa huru na haki.
Chisano ambaye pia ni rais wa zamani wa Msumbiji ameyasema hayo
mjini Nairobi katika mkutano wake na waandishi habari, baada ya kukutana
na maafisa wa serikali, makundi ya kijamii na IEBC.Akizungumza na waandishi habari baada ya kukutana na makundi hayo pamoja na viongozi wa vyama vya kisiasa, na kidini, Chisano alitoa wito kwa tume ya uchaguzi nchini Kenya kuhakikisha inashirikiana na taasisi nyingine muhimu ili kuhakikisha uchaguzi wa Machi 4 unafanyika kwa njia ya amani.
Joachim Chisano na Dr. Aisha Abdullahi
Kwa upande wake mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi na mipaka, Isaack Hassan, ametoa hakikisho kuwa maafisa wake tayari wamejipanga kukabiliana na uvunjaji wa kanuni zozote za uchaguzi.
Chisano ameandamana na mkuu wa masuala ya kisiasa wa Umoja huo, Dr. Aisha Abdullahi, ambaye atakuwa msaidizi wake kwenye shuhuli hiyo ya uangalizi wa uchaguzi mkuu nchini Kenya utakaofanyika siku ya jumatatu wiki ijayo.
No comments:
Post a Comment