Sunday, July 7, 2013

Wednesday, February 27, 2013

CHISANO ATOA WITO KWA IEBC

Kiongozi wa Ujumbe wa waangalizi wa Umoja wa Afrika, Joachim Chissano ameishauri tume huru ya uchaguzi nchini Kenya IEBC kushirikiana na vyombo vya usalama kuhakikisha uchaguzi ujao unakuwa wa huru na haki.
       Chisano ambaye pia ni rais wa zamani wa Msumbiji ameyasema hayo  mjini Nairobi katika mkutano wake na waandishi habari, baada ya kukutana na maafisa wa serikali, makundi ya kijamii na IEBC.

Akizungumza na waandishi habari baada ya kukutana na makundi hayo pamoja na viongozi wa vyama vya kisiasa, na kidini, Chisano alitoa wito kwa tume ya uchaguzi nchini Kenya kuhakikisha inashirikiana na taasisi nyingine muhimu ili kuhakikisha uchaguzi wa Machi 4 unafanyika kwa njia ya amani.
Joachim Chisano na Dr. Aisha Abdullahi  
Joachim Chisano na Dr. Aisha Abdullahi

Kwa upande wake mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi na mipaka, Isaack Hassan, ametoa hakikisho kuwa maafisa wake tayari wamejipanga kukabiliana na uvunjaji wa kanuni zozote za uchaguzi.
        Chisano ameandamana na mkuu wa masuala ya kisiasa wa Umoja huo, Dr. Aisha Abdullahi, ambaye atakuwa msaidizi wake kwenye shuhuli hiyo ya uangalizi wa uchaguzi mkuu nchini Kenya utakaofanyika siku ya jumatatu wiki ijayo.

Friday, February 15, 2013

MAHAKAMA KUU KENYA : hatuna uwezo kesi ya Kenyata,Rutto.

           Mahakama kuu ya Kenya imesema haina uwezo kisheria kuamua kama wagombea urais katika uchaguzi ujao nchini humo, Uhuru Kenyatta na mgombea wake mwenza William Ruto, waendelee kugombea au la.

Jopo la majaji watano wa mahakama hiyo, wamesema  kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kushughulikia suala linalohusu kugombea urais, wakisema ni mahakama ya juu kabisa pekee ambayo inao uwezo huo.
         Viongozi hao wa Muungano wa Jubilee wamepata afueni sasa baada ya Mahakama Kuu  kuhamishia kesi hiyo kwenye Mahakama ya Juu.
 
Mahakama hiyo imesema kwa kuwa tayari Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imeshakubali uteuzi wa Kenyatta na Rutto kushiriki kwenye uchaguzi mkuu ujao, mahakama hiyo haina mamlaka ya kubadilisha uamuzi wa IEBC.
         Mahakama hiyo imesma kwamba inao tu uwezo wa kuchunguza upya uamuzi wa IEBC kuhusu wagombea wengine lakini si wagombea urais na wagombea wenza wao. 
 ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 nchini KENYA.
 
Mahakama hiyo imesema kwamba wawili hao hawana hatia hadi watakapohukumiwa katika kesi yao inayowakabili huko The Hague na hakuna mtu anayeweza kubashiri iwapo wawili hao watapatikana na hatia.
          
Kesi hiyo ilifunguliwa na vyama vya kiraia vikipinga ushiriki wa wawili hao katika uchaguzi wa hapo tarehe 4 Machi, kwa madai kuwa wamekosa uadilifu kwa sababu wagombea hao tayari wamefunguliwa mashtaka ya kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).
         Mahakama hiyo imesema kwamba endapo mahakama ya ICC ingewasimamisha wawili hao kugombea nyadhifa za uongozi, basi hilo lingeliwezekana. Mahakama hiyo imeamua gharama ya washtakiwa kwenye kesi hiyo ilipwe na wenye kushtaki.